Chama cha madereva wa Malori nchini kimeeleza kusikitishwa na ongezeko la bei ya mafuta. Katibu Mkuu Dennis Kilia anasema kuwa ongezeko hilo litapandisha gharama za uendeshaji, jambo litakalowalazimu wasafirishaji hao kufikiria kuhamishia gharama hiyo ya ziada kwa wateja. Anaongeza kuwa wadau wa sekta ya usafirishaji watakutana ili kukubaliana kuhusu kiasi cha kupandisha ada za usafirishaji.


DENNIS KILIA - TRANSPORT