Uwanja wa Talanta utaandaa msururu wa HSBC Sevens 2 wikendi ya Januari tarehe 23-24 mwaka ujao, huku Nairobi ikikaribisha msururu wa kimataifa wa raga ya sevens kwa mwaka wa pili mfululizo. Shirikisho la Raga Duniani jana ilitangaza kwamba mji mkuu wa Kenya utaandaa mechi ya ufunguzi wa msururu wa mashindano matatu kabla ya kuhamia Montevideo, Uruguay na São Paulo, Brazil, kati ya Februari tarehe 20-28. Miji hiyo mitatu inarudi kama wenyeji baada ya kushiriki kwao katika shindano la kwanza la HSBC SVNS 2 mwaka huu.
Jua linashuhudiwa Mariakani, Mombasa na Kilifi.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.