Mwanamke mwenye umri wa miaka 35 alifariki huku mwingine akiachwa katika hali mahututi kufuatia tukio la kudungwa kisu katika nyumba ya kupangisha mjini Kajiado. Marehemu, aliyetambulika kwa jina la Mbithe, alithibitishwa kufariki alipowasili katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kajiado, ambako alikuwa amekimbizwa pamoja na mwathiriwa wa pili, mwenye umri wa miaka 49, polisi walisema. Polisi walisema tukio hilo lilitokea saa kumi na moja jioni jumatatu, katika nyumba ya kupanga inayomilikiwa na mwanamume mwenye umri wa takriban miaka 30.