Kenya imethibitisha kisa chake cha kwanza cha Ebola. Waziri wa Afya, Aden Duale, katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo, alisema mgonjwa huyo alikuwa raia wa Kenya aliyekuwa akiishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Duale alisema mgonjwa huyo alifariki  usiku wa kuamkia leo. Alikuwa akizungumzia utayari wa nchi hii kukabiliana na Ebola kufuatia kisa hicho kilichoripotiwa.