Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amewaonya wamiliki wa bunduki haramu katika eneo la Kerio Valley na maeneo jirani kusalimisha silaha zao la sivyo watakabiliwa na operesheni ya usalama inayolenga silaha haramu. Akizungumza huko Turkana, Murkomen aliwasihi wale wanaomiliki bunduki na silaha zingine haramu kuzisalimisha kabla ya zoezi la kusalimisha silaha lililopangwa kuanza, huku vyombo vya usalama vikizidisha juhudi za kukabiliana na ujambazi katika eneo hilo.

KIPCHUMBA MURKOMEN – CRACKDOWN