Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Justin Muturi anasema marehemu Raila Odinga alichukua nafasi muhimu katika mageuzi ya kisiasa nchini Kenya, kuanzia harakati za mfumo wa vyama vingi hadi utungaji wa Katiba ya mwaka 2010 na kipindi chake kama Waziri Mkuu. Wakati nchi ikijiandaa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Raila mnamo Oktoba 15, Muturi anasema kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa katika nyanja ya kisiasa ya Kenya.
JUSTIN MUTURI – RAILA