Askofu wa Kanisa la Anglikana huko Bondo, David Kodia, anasema kuwa kushindwa kwa upinzani kutoa usimamizi madhubuti kumewasukuma viongozi wa dini kuzungumzia masuala yanayowaathiri Wakenya. Askofu Kodia aliwalaumu viongozi wa upinzani kwa kuwaangusha wananchi, akisema kuwa ukosefu wao wa utulivu na umakini Bungeni umedhihirika huku Mamlaka ya Afya ya Jamii ikiendelea kukabiliwa na changamoto. Aliwataka viongozi hao kushughulikia masuala yanayowatia wasiwasi Wakenya.

DAVID KODIA – LEADERS