Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen anasema zaidi ya Wakenya milioni 4.6 wenye umri kati ya miaka 15 na 65 wanatumia angalau dawa moja ya kulevya au kitu kingine. Akinukuu data ya NACADA, Murkomen anasema eneo la Pwani linasalia kuwa miongoni mwa yaliyoathiriwa zaidi, huku Mombasa ikirekodi kiwango cha juu zaidi nchini kwa asilimia 34.4. Anasema serikali inachanganya utekelezaji na kinga, matibabu na ukarabati ili kushughulikia matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

KIPCHUMBA MURKOMEN – DRUGS