Wakenya wametakiwa kuacha kuwanyanyapaa watu wanaoishi na matatizo ya afya ya akili, hasa vijana. Daktari William Mbaabu anasema ukosefu wa elimu bado ni changamoto kubwa katika kushughulikia masuala ya afya ya akili ndani ya jamii. Anatoa wito wa kuongezwa kwa elimu kwa umma ili kuboresha ueledi kuhusu magonjwa ya akili na kuwahimiza watu walioathirika kutafuta msaada. Mbaabu anasema unyanyapaa unaweza kuwazuia watu wengi kupata huduma na msaada unaohitajika.
WILLIAM MBAABU – STIGMA