Chama cha UDA kimebadilisha tarehe za uchaguzi wake wa ngazi ya wadi katika kaunti 13, huku wanachama husika wakitarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo mwezi Oktoba. Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi ya chama hicho kupitia taarifa, ilisema kuwa imepitia upya mpango wa uchaguzi na kurekebisha ratiba iliyotangazwa awali tarehe 12 Septemba. Tarehe hizo zilizorekebishwa zinachukua nafasi ya ratiba ya awali kwa kaunti husika, ambapo sasa uchaguzi huo utafanyika tarehe 2, 3, 16 na 17 Oktoba.