Wahadhiri katika vyuo vikuu vya umma wanatarajiwa kugoma kuanzia Oktoba tarehe 2 baada ya Chama chao UASU kutoa notisi ya mgomo wa kitaifa ya siku saba. Katibu Mkuu wa UASU Constantine Wasonga alisema hatua hiyo inafuatia kushindwa kwa serikali kutekeleza CBA ya 2025-29. Wasonga alisema SRC iliarifu vyama vya vyuo vikuu kwamba Wizara ya Elimu wala Hazina haikuwa imetoa uhakikisho wa maandishi kwamba ufadhili wa CBA utatolewa kupitia Hazina ya Kitaifa.

CONSTANTINE WASONGA - UNDERSTAFFED