Ureno ilianza utetezi wao wa taji la Nations League kwa ushindi mgumu wa 1-0 dhidi ya Wales wakati Cristiano Ronaldo aliporejea Lisbon tangu alipoanza kucheza mechi yake ya kwanza miaka 24 iliyopita. Jitihada za Joao Felix dakika ya 22 zilitosha kuwapatia ushindi mbele ya mashabiki wa nyumbani. Wakati huo huo, Cody Gakpo alifunga bao la kusawazisha dakika za mwisho na kufuta bao la kwanza la Felix Nmecha kipindi cha kwanza huku Uholanzi ikilazimisha sare ya 1-1 na Ujerumani, Ugiriki ikiishinda Serbia 2-1 na osovo ikiishinda Ireland 1-0. Kwingineko, Erling Haaland alifunga mabao mawili huku Norway ikiishinda Denmark 3-2, Austria ikiishinda Israel 3-1 nayo Malta ikiishinda Andora 2-1.
Baada ya miaka mingi ya uvumi, mazungumzo, na majaribio tofauti ya kufanya pambano hilo lifanikiwe, Tyson Fury na Anthony Joshua hatimaye wataingia ulingoni. Mpambano uliotarajiwa sana kati ya majina mawili makubwa katika kitengo cha uzito wa juu ulithibitishwa rasmi jana na promota wa Saudia Turki Alalshikh. Kulingana na Turki ni mojawapo ya mapambano makubwa zaidi ambayo yanaweza kupangwa katika ndondi, baada ya takriban miaka 15 ya majaribio yaliyoshindwa kuwaleta Fury na Joshua pamoja ulingoni.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.