Alex Mwangi atakuwa akilenga kupata ushindi wa pili mfululizo katika msururu wa mashindano ya Kenya Amateur Golf Championship wikendi hii, wakati wa mashindano ya NCBA Nanyuki Open yatakayofanyika katika Klabu ya Michezo ya Nanyuki kuanzia leo hadi Jumapili. Mchezaji huyo wa Klabu ya Gofu ya Windsor alipata ushindi wake wa kwanza katika msururu huo wikendi iliyopita kwenye mashindano ya NCBA Diani Beach Masters, akirekodi alama 218 kupitia raundi za 76, 71 na 71, na kumaliza akiwa na faida ya mikwaju mitatu mbele ya Eugene Wafula. Zawadi ya Shilingi 500,000 za Kenya itakuwa iking'ang'aniwa.

 

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Naivasha, Gilgil na Narok.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.