Serikali inasema mali zinazotumika au kupatikana kupitia biashara haramu ya dawa za kulevya na biashara haramu ya pombe zitachukuliwa kama mapato ya uhalifu na kulenga kufungiwa na kupeanwa. Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen anasema Rais ameagiza kwamba mali zilizopatikana zielekezwe kwenye programu za ukarabati, kinga na matibabu. Murkomen anasema serikali pia italenga majengo na ardhi inayotumika kutengeneza au kuhifadhi dawa haramu na pombe.

KIPCHUMBA MURKOMEN – ASSETS