Seneta mteule Hamida Kibwana ameiomba Kamati ya Seneti ya Afya kutoa taarifa kuhusu uhaba wa mbinu na bidhaa za kupanga uzazi humu nchini. Anasema kuwa bidhaa tisa kati ya 13 muhimu za kupanga uzazi hazipatikani katika shirika la KEMSA, zikiwemo dawa za sindano na zile za kumeza, huku akina mama wanaonyonyesha wakiathirika zaidi na uhaba wa vidonge vyenye homoni ya 'progestin' pekee.
HAMIDA KIBWANA – SHORTAGE