Rais William Ruto ametoa wito wa mbinu mpya ya maendeleo ya Afrika, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano unaozingatia uwekezaji, uongezaji thamani na ustawi wa pamoja badala ya misaada ya kifedha na uchimbaji wa rasilimali pekee. Akizungumza jijini New York katika Baraza la ECAM, Ruto alisema Kenya iko tayari kupokea uwekezaji unaozalisha ajira, kuhamisha teknolojia, kujenga ujuzi na kuimarisha taasisi za Afrika. Alisisitiza haja ya ushirikiano unaoleta fursa za kiuchumi za muda mrefu na maendeleo endelevu kote barani humo.
WILLIAM RUTO-INVEST