Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana nchini, Jackson Ole Sapit, ameonya kuhusu kuzidi kuwa mbaya kwa changamoto nchini, akitaja kutovumiliana kisiasa, huduma za afya zilizolemewa, ukosefu wa ajira, gharama kubwa ya maisha na kupanda kwa kodi. Sapit alionya kuwa hali hiyo inaweza kuzidi kuwa mbaya zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, huku akiitaka serikali kushughulikia changamoto hizo kwa dharura ili kuzuia hali hiyo kuwa mbaya zaidi.

 JACKSON SAPIT - REVIEW