Chama cha ODM kimesema kitamuunga mkono Gavana wa Kajiado, Joseph Ole Lenku, katika azma yake ya kuwania nafasi ya Seneta wa kaunti hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama hicho ambaye pia ni Gavana wa Homa Bay, Gladys Wanga, anasema Lenku anastahili kuungwa mkono na chama hicho huku akihitimisha muhula wake wa pili kama gavana.
GLADYS WANGA – LENKU