Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Majanga (NDOC) kimetoa tahadhari kuhusu mvua inayotarajiwa kunyesha kwa kiwango cha juu kuliko kawaida kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba, na kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka ujao. Mkurugenzi wa kituo hicho, David Samoei, anaonya kuwa mvua hiyo inaleta hatari kubwa ya mafuriko na maporomoko ya ardhi, huku akibaini kuwa mamlaka zinaimarisha maandalizi ya dharura yakilenga maeneo yaliyo katika hatari kubwa kote Kaskazini-Mashariki mwa Kenya, maeneo ya pwani na bonde la Ziwa Victoria.
DAVID SAMOEI – FLOODS