Aliyekuwa msemaji wa serikali, Isaac Mwaura, ametoa wito wa kuendelezwa kwa juhudi za utetezi ili kuhakikisha kuwa haki za watu wenye ulemavu wa kusikia zinatekelezwa kikamilifu. Mwaura anasema kwamba kuwa na sheria na sera pekee hakutoshi, huku akionya kuwa mafanikio yaliyopatikana katika nyanja ya haki za watu wenye ulemavu yanaweza kupotea iwapo hakutakuwa na hatua endelevu. Anasema Lugha ya Ishara ya Kenya (KSL) inapaswa kutumiwa sana katika mawasiliano ya umma, na kwamba kuwa na uelewa mpana wa lugha hiyo kutawasaidia Wakenya kuwasiliana na watu wenye ulemavu wa kusikia wakati wa dharura.
ISAAC MWAURA – VIGILANCE