Mkurugenzi wa shirika la Vocal Africa, Hussein Khalid, amefichua kuwa mwanaharakati Muteti Mulinge, ambaye alikuwa ametoweka, amepatikana eneo la Lukenya. Khalid alisema kuwa Muteti alipatikana baada ya kutelekezwa katika eneo hilo majira ya saa tisa alfajiri ya leo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwanaharakati huyo ilimbidi kutembea umbali mrefu kabla ya kufika kituo cha mafuta, ambapo alikutana na msamaria mwema aliyemsaidia kupata simu, na akawasiliana na kakake na kuijulisha familia yake kuhusu mahali alipo.