Kundi la maseneta linapendekeza kukabidhiwa kwa serikali za kaunti jukumu la kusimamia baadhi ya mbuga za kitaifa za wanyamapori na maeneo yaliyohifadhiwa. Maseneta hao, wakiongozwa na Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’, wanasema hatua hiyo itawezesha kaunti kunufaika zaidi na mapato yatokanayo na utalii. Wanahoji kuwa mbuga za wanyamapori na maeneo yaliyohifadhiwa ni rasilimali muhimu zinazoweza kuingizia kaunti mapato ya ziada na kuchochea maendeleo ya eneo husika.


VOX POP-REVENUES