Maseneta jana walihitimisha mpango wa 'Senate Mashinani' katika Kaunti ya Kilifi. Mpango huo, uliofanyika katika Bunge la Kaunti ya Kilifi, ulijumuisha vikao rasmi vya bunge, vikao vya kamati, mikutano na wananchi, pamoja na ziara katika miradi na taasisi mbalimbali. Kilifi ilikuwa kaunti ya tano kuandaa vikao vya Seneti nje ya Nairobi, ikifuatia Uasin Gishu (2018), Kitui (2019), Turkana (2023) na Busia (2025).