Aliyekuwa mseamaji wa serikali, Isaac Mwaura, anasema kuwa watu wenye ulemavu wanaandaa Ajenda ya Pamoja ya Masuala ya Ulemavu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Mwaura anasema mpango huo unajengwa juu ya ajenda yenye vipengele 10 iliyoandaliwa kupitia mashauriano na makundi ya watu wenye ulemavu, na unalenga kupata ahadi kutoka kwa viongozi wa kisiasa wa mirengo mbalimbali. Anasema lengo ni kupata mpango wa pamoja wa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa katika masuala ya utawala.

ISAAC MWAURA – MANIFESTO