Wanachama wa KNUT katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wametishia kugoma baada ya kudai kuwa Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) ilihamisha michango yao ya chama kwa chama cha KUPPET bila idhini yao. Walipinga hatua hiyo, wakiiita "uhamishaji wa lazima" au "kunyakuliwa" kwa wanachama wao na TSC, na kuipa tume hiyo muda hadi mwezi Oktoba kubatilisha uhamisho huo unaodaiwa. Walisema walimu walioathirika walishangaa walipopokea hati zao za malipo ya mwezi Septemba na kugundua kuwa michango yao ya chama ilikuwa imewasilishwa kwa KUPPET.
VOX POP – MEMBERS