Kanisa la Anglikana Nchini limeitaka Serikali kuimarisha uwajibikaji, kutetea haki za binadamu na kushughulikia ufisadi, likionya kwamba nchi haiwezi kufikia mshikamano wa kitaifa huku raia wakiendelea kukabiliwa na ugumu wa kiuchumi, dhuluma na mivutano ya kisiasa. Askofu Mkuu Jackson Ole Sapit anasema Kanisa haliwezi kubaki kama mtazamaji wakati raia wanateseka, akiwahimiza viongozi kudumisha haki, uadilifu na utawala unaowajibika.
JACKSON OLE SAPIT – CITIZENS