Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, ameihimiza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027 unakuwa huru na wa haki, huku akionya dhidi ya kujirudia kwa hali aliyoielezea kama uchaguzi ulioibwa. Kalonzo alisema mjadala kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2022 unapaswa kuendelea na kuitaka IEBC kudumisha msimamo wa kutopendelea upande wowote katika kusimamia uchaguzi huo.

 KALONZO MUSYOKA – IEBC