IEBC inasema inaendeleza hatua za kufanya Uchaguzi Mkuu wa 2027 uwe jumuishi zaidi na shirikishi, hasa kwa watu wenye ulemavu. Kamishna Ann Nderitu anasema Tume hiyo imeanzisha Kamati za Ujumuishaji wa Watu Wenye Ulemavu katika kaunti zote 47 na katika ngazi ya kitaifa, huku pia ikiwafunza wataalamu wa vyombo vya habari kuhusu kuripoti uchaguzi unaozingatia ulemavu. Anasema Tume hiyo itafanya kazi na jamii ya walemavu wa kusikia na wawakilishi wao kabla ya usajili ulioboreshwa wa wapiga kura ili kutambua na kushughulikia vikwazo vya ushiriki.

ANN NDERITU – INCLUSIVITY