Madereva wanaotumia barabara ya Southern Bypass na barabara nyingine muhimu jijini Nairobi watakumbana na usumbufu Jumapili hii wakati jiji likiandaa mashindano ya baiskeli ya 'Grand Nairobi Race'. Mkuu wa trafiki jijini Nairobi, Bossmack Kungu, alisema kuwa barabara ya Southern Bypass, sehemu za Barabara ya Ngong katika makutano ya Lenana, eneo la Uhuru Gardens na barabara ya kuelekea Carnivore zitafungwa kuanzia saa sita usiku hadi saa saba mchana. Mashindano hayo yatawakutanisha waendesha baiskeli wa mashindano, timu, waendesha baiskeli wenye ulemavu, familia na watoto. Huyu hapa ni Peter Kibe kutoka kundi la Jubilee.

PETER KIBE-RACE