Unga wa mahindi na ngano ni njia bora ya kuwapa watu vitamini na madini muhimu kama vile madini ya iron, zinki, na vitamini A. Hii huwasaidia watu kupata virutubisho wanavyohitaji bila kubadilisha milo yao ya kila siku. Akizungumza katika kongamano la Chama cha Wasaga Nafaka jijini Nairobi, mtaalamu wa lishe na sayansi ya chakula, Peter Kahenya, aliwahimiza wasagaji nafaka na wadau wa sekta hiyo kukumbatia uongezaji wa virutubisho kwenye chakula kama njia muhimu ya kupambana na njaa iliyojificha na utapiamlo.


 PETER KAHENYA – FORTIFICATION