Waziri wa Michezo Salim Mvurya, anasema kuwa karibu wanufaika elfu 15 wa kundi la kwanza la mpango wa NYOTA wanangoja kupewa nafasi katika programu za mafunzo ya ujuzi kazini Mvurya anasema mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 20 Aprili mwaka ujao, kufuatia kukamilika kwa mchakato wa kuingiza mashirika yatakayotoa mafunzo hayo. Anaeleza kuwa maandalizi ya makundi yaliyosalia yamekamilika, huku mikataba na watoa huduma ikiwa imetiwa saini na mpango wa utekelezaji ukipangwa kufanyika katika kipindi cha miezi miwili.

SALIM MVURYA – NYOTA