Mwenyekiti wa EACC Askofu David Oginde anasema ufisadi unachangia miradi isiyokamilika, vituo vya afya visivyotosha na miundombinu ya umma iliyochakaa. Askofu Oginde anasema uhamishaji wa rasilimali za umma katika mifuko ya watu binafsi unawanyima Wakenya huduma na maendeleo muhimu. Anasema Kenya ina uwezo wa kufikia viwango vya maendeleo sawa na Singapore ikiwa ufisadi utashughulikiwa ipasavyo, akiwahimiza raia kujiunga na vita dhidi ya ufisadi.

DAVID OGINDE – CORRUPTION