Timu ya taifa ya Eritrea iliwasili nchini Kenya Jumanne kujiandaa kwa mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2027 dhidi ya Harambee Stars itakayochezwa Jumamosi. Timu hiyo ilifanya mazoezi yake ya pili katika Uwanja wa Police Sacco jioni hii, na itafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja utakaotumika kwa mechi hiyo, Uwanja wa Nyayo, kesho. Eritrea itakuwa ikijaribu kuwashangaza wenyeji Kenya katika mechi hiyo, baada ya kuifunga Stars mabao 4-1 katika nusu fainali ya mashindano ya CECAFA mwaka 2019 jijini Kampala, Uganda.




Jua linashuhudiwa Makindu, Voi na Mariakani.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.