Waziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, anasema serikali inaangazia upya maslahi ya polisi wa akiba, ikiwemo kuongeza marupurupu yao ya kila mwezi kutoka shilingi elfu tano hadi elfu kumi. Murkomen anasema serikali pia inashughulikia kuwasajili wanachama wote wa kikosi hicho katika mpango wa SHA na kuwapatia sare na vifaa vinavyofaa. Alisema rasimu ya sera kuhusu usimamizi na uratibu wa kikosi hicho imefikia hatua ya juu na hivi karibuni itawasilishwa mbele ya Baraza la Mawaziri.
KIPCHUMBA MURKOMEN – WELFARE