Waziri wa Michezo Salim Mvurya, anasema serikali imeweka afya ya akili na ustawi wa jumla kama kipaumbele cha kimkakati kwa vijana wabunifu na nguvukazi kwa ujumla. Akiwa mbele ya Seneti, Mvurya alisema Kenya haina takwimu za kina kuhusu visa vya kujiua na matatizo ya afya ya akili miongoni mwa wasanii na waundaji wa maudhui. Alitaja ukosefu wa uthabiti wa kifedha, ufuatiliaji wa karibu wa umma mitandaoni, unyanyasaji wa mtandaoni na shinikizo la kuendelea kuwa na mvuto au umuhimu katika tasnia, kama changamoto kuu.
SALIM MVURYA – MENTAL HEALTH