Kiongozi wa ODM, Oburu Oginga, amemjibu Rais wa zamani Uhuru Kenyatta kufuatia madai yake kwamba Raila Odinga alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2022. Oburu alihoji ni kwa nini Uhuru alisubiri karibu miaka minne kabla ya kutoa kauli hizo. Alisema kuwa ODM ilikuwa tayari imeamua kusonga mbele baada ya kutumia rasilimali nyingi kupinga matokeo ya uchaguzi huo. Pia, Oburu alimkosoa Uhuru kwa kukabidhi madaraka kwa Rais William Ruto licha ya kudaiwa kufahamu kuwepo kwa kasoro na udanganyifu katika uchaguzi huo wa 2022.