Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amewaonya Polisi wa Kitaifa wa akiba dhidi ya kutumia vibaya silaha zao, akisema wanakabiliwa na hatua kali za kinidhamu na kisheria ikiwa watavunja sheria. Akizungumza katika Kaunti ya Meru wakati wa sherehe ya kufuzu kwa polisi wa akiba 705, Murkomen alisema silaha zao zinalenga kuwalinda Wakenya katika jamii zote na sio kuchochea migogoro. Aliwasihi kutumia kiwango cha juu cha nidhamu na uwajibikaji.
KIPCHUMBA MURKOMEN – WARNING