Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amewaonya wanasiasa dhidi ya kuwapa silaha na kuwatumia magenge kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Waziri Murkomen anasema serikali inawafuatilia kwa karibu watu binafsi wanaohusika katika shughuli hizo na itachukua hatua dhidi yao. Aliwaonya watendaji wa kisiasa dhidi ya kutumia vikundi vya uhalifu kusababisha vurugu au kutishia jamii, akisema vyombo vya usalama vitawachukulia hatua wale watakaopatikana wakiwezesha au kufadhili vikundi hivyo.
KIPCHUMBA MURKOMEN – POLITICIANS