Kiongozi wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, anatarajiwa kuendelea na msururu wa shughuli za kukutana na umma katika kaunti za Kitui, Busia na Siaya. Leo, Kalonzo atarejea nyumbani kwake Tseikuru, Kaunti ya Kitui, ambapo ataongoza familia yake katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 tangu kufariki kwa mama yake, Marehemu Mama Sarah Musyoka. Kisha, Kalonzo atasafiri hadi Kaunti ya Busia siku ya Jumamosi kabla ya kuhudhuria ibada kanisani huko Bondo, Kaunti ya Siaya, siku ya Jumapili.