IEBC imepanga kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa MCA  katika Wadi ya Migwani, eneo bunge Mwingi Magharibi, Kaunti ya Kitui, mnamo tarehe 17 Novemba 2026. Mwenyekiti wa IEBC, Erastus Ethekon, alisema uchaguzi huo unafuatia kutangazwa kwa nafasi hiyo kuwa wazi na Spika wa Bunge la Kaunti hilo mnamo tarehe 6 Agosti. Nafasi hiyo ilibaki wazi baada ya Harrison Mawia kujiuzulu kama MCA ili kushika wadhifa wa Karani wa Bunge la Kaunti ya Kitui.