Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, anadai kuwa Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, atatumia chama cha UDP kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Katika machapisho kwenye mitandao ya kijamii, Natembeya alisema Sifuna pia atahudumu kama kiongozi wa chama hicho na mgombea urais. Madai hayo yanakuja wakati Sifuna akijiandaa kuzindua jukwaa lake jipya la kisiasa mapema mwezi ujao. Hivi karibuni, Msajili wa Vyama vya Siasa alikataa ombi la Sifuna na Natembeya la kubadilisha jina la UDP na kuwa Ukombozi Party of Kenya.