Wamiliki wa baa wanatoa wito wa kupigwa marufuku ya miezi sita kwa pombe za aina ya 'second-generation' ili kudhibiti vinywaji ghushi sokoni. Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Baa, Simon Njoroge, anasema kuwepo kwa pombe hizo kumechangia vifo vinavyohusishwa na vinywaji haramu, huku akilaumu udhaifu katika utekelezaji wa sheria na kanuni na mashirika kama KEBS, NACADA, polisi na mamlaka nyingine kwa kuendelea kwa tatizo hilo.
SIMON JIROGE - GENERATION ALCOHOL