Mahakama Kuu jijini Nairobi itatoa uamuzi mnamo Februari mwaka ujao kuhusu ombi linalotaka kuilazimisha IEBC kufanya mapitio ya muda mrefu ya mipaka ya maeneo bunge na wadi. Philip Kipkemoi aliwasilisha kesi mahakamani kupitia wakili wake Felix Keaton, akisema kwamba Tume hiyo imeshindwa kuzingatia wajibu wake wa kikatiba chini ya Kifungu cha 89 wa kupitia upya mipaka ya uchaguzi mara kwa mara.

FELIX KEATON – IEBC