Viongozi wa Narok wametakiwa kuacha siasa za mgawanyiko na kukuza umoja miongoni mwa wakaazi licha ya tofauti zao za kisiasa. Seneta wa Nyandarua, John Methu, ambaye aliwasilisha ajenda ya upinzani huko Ntulele, aliwataka viongozi kuhubiri amani na kuhakikisha jamii zinaendelea kuwa na umoja. Methu alisema tofauti za kisiasa hazipaswi kuruhusiwa kuleta migawanyiko miongoni mwa wakaazi au kudhoofisha mshikamano huko Narok.

JOHN METHU – LEADERS