Mashindano ya LOOP Safari Gravel Series yatafanyika Nanyuki kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi, tarehe 17 Oktoba, ikiwa ni awamu ya nne ya msururu wa mwaka huu, huku waendesha baiskeli 600 wakitarajiwa kushiriki. Mashindano hayo ya Nanyuki yatahusisha Njia ya Chui (kilomita 11), Njia ya Duma (kilomita 45), na Njia ya Simba (kilomita 90) kwa ajili ya washiriki wa daraja la juu (elite). Washiriki watatu wa kwanza katika mbio za daraja la juu za kilomita 90 watajipatia zawadi za pesa taslimu sh elfu 20, KES 15,000 na KES 10,000 mtawalia. Timu itakayoshinda itajipatia KES elfu 125, huku timu zitakazoshika nafasi ya pili na ya tatu zikipokea KES 100,000 na sh elfu 70 mtawalia.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Makindu, Voi na Mariakani.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.