Kuna hali ya mvutano katika kambi ya timu ya Harambee Stars kabla ya mechi yao ya kufuzu kwa AFCON mwaka 2027 dhidi ya Eritrea siku ya Jumamosi. Hali hii imejitokeza baada ya wachezaji kugoma kufanya mazoezi jana, wakilalamikia kutolipwa marupurupu, mazingira duni ya ustawi, na changamoto za kiutendaji wakati wa mechi zao za kimataifa. Wachezaji hao wanadai kuwa wamekuwa wakikaa katika hoteli zisizokidhi viwango na mara nyingi wamekuwa wakisafirishwa kwa ndege za bei nafuu zinazohusisha kusubiri kwa muda mrefu. Pia wanataka kulipwa marupurupu yote ambayo bado hayajalipwa kabla ya kurejea mazoezini.
Vipindi vy anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.