Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, ameishutumu serikali ya Kenya Kwanza kwa kushindwa kuwekeza ipasavyo katika miundombinu na usalama jijini humo. Sifuna alisema ni jambo la kusikitisha kwamba viongozi wa Kenya wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wanaweza kutembea kwa uhuru katika mitaa ya New York, lakini hawawezi kufanya hivyo jijini Nairobi kutokana na ukosefu wa usalama na hali mbaya ya njia za watembea kwa miguu. Aliyasema hayo wakati wa kikao cha tano cha 'Senate Mashinani' huko Kilifi.
EDWIN SIFUNA – WALK