Serikali inaongeza juhudi za uratibu na maandalizi ili kuokoa maisha na kulinda mali wakati wa utabiri wa mvua kubwa kati ya Oktoba na Disemba. Naibu Rais Kithure Kindiki anasema serikali za kitaifa na za kaunti, washirika wa maendeleo na mashirika ya kibinadamu yanatekeleza hatua za kukabiliana na maafa katika maeneo yanayokabiliwa na majanga. Anasema vituo vya mijini, ikiwa ni pamoja na Nairobi na Mombasa, vinapata kipaumbele maalum ili kupunguza mafuriko ya ghafla na hatari zingine zinazohusiana na mvua kubwa.
KITHURE KINDIKI – RAINS