Rais William Ruto ametoa wito wa kufanyiwa marekebisho kwa mfumo wa kifedha, akisema kuwa Afrika inahitaji fedha zenye gharama nafuu, dhamana imara na mifumo ya kujua hatari ili kuchochea uwekezaji, kuunda ajira na kujenga ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Akizungumza jijini New York, Ruto alisema kuwa malengo ya Afrika kuhusiana na haliya hewa hayawezi kufikiwa bila kushughulikia changamoto za kifedha. Aliutaka ulimwengu kuuchukulia utekelezaji wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kama fursa ya ukuaji, ustahimilivu na kulinda jamii.
WILLIAM RUTO – ASSISTANCE