Rais William Ruto anatarajiwa kutoa hotuba kuu ya Kenya katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York leo. Ruto, amefanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa dunia na kushiriki katika mikutano inayohusu teknolojia, maendeleo na ushirikiano wa kimataifa; pia amekutana na Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani, Marco Rubio. Ruto amesisitiza haja ya kufanyika kwa mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na taasisi za fedha za kimataifa, akitoa wito wa kuwepo kwa uwakilishi mkubwa zaidi wa Afrika katika michakato ya kimataifa ya kufanya maamuzi na masuala ya teknolojia.